Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa yatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 20/06/2017.
Mwenge huo wa Uhuru unatarajiiwa kupokelewa katika eneo la Mwanakianga kata ya Mazae ukitokea Wilayani Kongwa. Baada ya kupokelewa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, huku ukizindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali. Baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Mpwapwa mwenge huo utakesha katika kijiji cha Chipogoro kata ya Chipogoro. Siku ya tarehe 21/06/2017 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa wilaya ya Chamwino.
Wananchi wote mnakaribishwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.