Watoto wa Wilaya ya Mpwapwa leo katika kuadhimisha Sherehe za Siku ya Mtoto Afrika wamelalamikia mambo mbalimbali yanayofanywa na watu wazima ambayo kwa namna moja au nyingine yanaathiri ukuaji wao kiakili, kisakolojia, kimwili na kiroho. Baadhi ya mambo yaliyolalamikiwa ni pamoja na wanawake kutoa mimba au kutupa watoto baada ya kujifungua, kutoa adhabu kali kwa watoto wanapokosea mpaka kusababisha kupoteza maisha au kupata kilema kwa baadhi ya watoto, mimba na ndoa za utotoni, na kuwanyima haki ya msingi kama kwenda shule kwa kuwapa kazi za kuuza biashara.
Akisoma risala Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Ihala kwa Mgeni rasmi Ndugu. Obert Mwalyego Afisa Tarafa ya Mpwapwa Mjini akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ambaye alikuwa katika majukumu mengine ya kiserikali, imeelezwa kuwa "Katika kusherekea siku hii ya Mtoto Afrika inakumbukwa kuwa mwaka 1992 watoto zaidi ya elfu moja waliua na Makaburu huko Afrika ya Kusini katika mji wa SOWETO baada ya watoto kufanya maandamano ya kupinga kubadilishwa kwa mtaala wa masomo kuwa kwa lugha ya kigeni". Pia katika risala hiyo imeeleza kuwa katika Nchi yetu ya Tanzania watoto wanafanyiwa ukatili wa kubakwa, kupewa adhabu kali, kulawitiwa, kufanyishwa kazi ngumu, kutopewa muda wa kucheza na kupumzika.
Mgeni rasmi Ndugu. Obert Mwalyego (katikati) akiwa na Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu. khamlo Njovu (kulia) na Mhe. Madanya diwani wa Kata ya Mazae (kushoto)
Hata hivyo katika sherehe hizo watoto waliamua kubeba mabango yaliokuwa na ujumbe kama Mtoto ana haki ya kuishi, kuendelezwa, kulindwa, kushirikina kutobaguliwa ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wazazi na walezi wanao wanyima haki zao za msingi.
Aidha katika maigizo yaliyotolewa na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Chazungwa Juu ya Ukali wa Watoto: Mwanafunzi anaomba fedha ya ada ya shule, baba mzazi anamtukana mtoto na kumwambia kama anataka aache shule maana haoni umuhimu wa shule, shuleni pia mwanafunzi huyo anatolewa darasani na kupewa adhabu ya viboko kwa kukosa ada wakati jukumu la kulipaada ni la mzazi. Kwa kuliona hilo ndio maana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefuta michango ya ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne kwa kuwajali watoto.
Mgeni rasmi na mea kuu wakipiti kila meza kujionea kazi za sanaa zinazofanywa na watoto wa Mpwapwa
Vile vile katika igizo lilitolewa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mazae Juu ya Haki za Watoto: Igizo lilionyesha kuwa kunabaadhi ya wazazi huwakataza watoto wao wasiendeshule na kuwatuma kuuza biashara ili kupata kipato cha familia wakati baba na mama wakiwa wameenda shamba kulima. Pia katika igizo hilo mwanafunzi alitambua haki zake na kwenda polisi akiwa anauza vitumbua kuwashitaki wazazi wake ili wasiwe wanamtuma kufanyabiashara na kumkataza kwenda shule. Hatimaye mwanafunzi alipata haki ya kuhudhurua shule na kufaulu vizuri.
Katika sherehe hizo watoto walionyesha kazi za sana za mikono kama kufuma vitambaa, kushona viatu na kucheza muziki. Kwa kutambua watoto wanapaswa kuwa wabunifu na kupata muda wa kucheza, katika siku hii watoto wamefurahi kuwa kuimba na kuonyesha vipaji vya kusoma na kucheza.
Watoto wakiwa katika igizo la Ukatili Dhini ya Watoto mbele ya meza kuu
Mwisho mgeni rasmi ameagiza vyombo vya dola na mamlaka zinazoshughulikia haki za watoto kuwasikiliza, kuwaelimisha na kuwapa msaada wanapohitaji. Pia kuwachukulia hakua watakaowafanyia ukatili watoto pamoja na wale watakaowanyima haki zao.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.