Wananchi Wilayani Mpwapwa wameiomba Serikali kusaidia kukarabati miundombinu ya bara bara hususani katika kipindi hiki ambacho mvua zinazoendelea kunyesha zimeharibu miundombinu ya bara bara kiasi ambacho kuna baadhi ya maeneo yamekuwa hayapitiki kwa urahisi. Diwani wa kata ya Mlunduzi Mhe Orgenes Mchete John anatanabaisha kuwa kwa mfano katika kata ya Mlunduzi hali ya bara bara ni mbaya na kumekuwa na changamoto ya kimawasiliano baina ya vijiji vya Chinyang'uku, na Chinyika kutokana na uharibifu mkubwa wa bara bara na vivuko zaidi ya saba ambavyo ukarabati wake unahitaji kiasi cha Sh 1,800,000,000.00 kwa mujibu wa Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya Eng. Boniphace Makiya. Naye Mhe. Richard Maponda Diwani wa Kata ya Luhundwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Uchumi amepongeza jitihada za Serikali katika kutatua changamoto za bara bara kwa kutoa fedha za ukarabati katika bajeti na Matengenezo ya Dharula lakini ameomba serikali iendelee kutoa fedha zaidi ili miundombinu iboreshwe na kurahisisha mawasiliano.
(Bara bara iliyoharibiwa na mvua katika Mojawapo ya maeneo korofi ya Bara bara ya Kidenge)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.