Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amefanya kikao na Wadau wa Biashara katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo. Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa nyumba za kulala wageni, wafanyabiashara wa maduka, mazao na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria na mizigo pamoja na wataalam toka sekta ya umma. Katika kikao hicho wafanyabiashara wamemueleza mkuu wa wilaya kuwa changamoto kubwa ni ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma ni mdogo na kusababisha wadau wa sekta binafsi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mambo muhimu katika kuendesha biashara zao.
Wadau wa Biashara wakiwa katika kikao cha pamoja katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa na kujadili changamoto za biashara
Pia wadau wa sekta binafsi kwa pamoja wamemshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Shekimweri kwa kuwakutanisha na wadau wa sekta za umma pamoja na wataalam mbalimbali. Hivyo wadau hao wa sekta binafsi wameelezwa mambo muhimu katika uanzishwaji wa biashara mbalimbali na hatua zake za msingi. Pia wadau wa biashara wameelezwa kuwa katika kuanzisha biashara flani, inategemeana aina ya biashara ni vema kupata ushauri toka kwa mamlaka husika, kisha taratibu za kutafuta TIN na leseni ya biashara zinafuata.
Wadau wa Biashara wakiwa katika kikao cha pamoja katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa na kujadili changamoto za biashara
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri amewaagiza wadau na wataalam mbalimbali wanaosimamia masuala ya biashara hapa Wilayani kama vile Afisa Biashara, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Uthibiti wa Chakula na Dawa, Afisa Usafi na Mazingira, Afisa Afya na Afisa Misitu na Maliasili kuwapatia elimu na kuwajengea uelewa wa kutosha wafanyabiashara ili wawezesha kufanya biashara kwa kufuata sheria na taratibu na kupata faida staiki ili kuweza kulipa kodi na ushuru kwa wakati bila usumbufu wowote.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.