Jumla ya wanavikundi mia tatu ishirini wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa watanufaika na mkopo wa asilimia 10, kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.
Juni 13,2025 wamepokea hundi ya Fedha ya Sh.286,800,000 kwa ajili ya kupatiwa mikopo hiyo waliyoomba yenye lengo la kuendeleza Shuhuli mbali mbali na kuweza kujiingizia kipato kitakachoweza kuleta faida na kuweza kurejesha malipo kwa haraka.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya Mh.Dkt Sophia Mfaume Kizigo ametoa agizo kwa Mkurugenzi na Halmashauri yake ni kuhahakikisha wanawafatilia katik biashara zao ili wasikwame lna waweze kufanikiwa katika biashara hizo na iwe rahisi kurejesha deni lao.
Mwisho amewaasa wana vikundi viache migogoro mara tu baada ya kupewa mikopo na badala yake watumie mikopo hiyo kuwaendeleza kimaendeleo ili waweze kufikia lengo,na kuwaombea mafanikio ili waweze kufanikiwa na kukwamukwa kiumaskini.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.