Maadhimisho ya Siku ya Uhuru Tanzania leo Disemba 09,2024 wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakiongozwa na Mh Dkt Sophia Kizigo wamepanda miti zaid ya mia saba katika Eneo la Ujenzi wa Shule mpya ya Mbuyuni ili kuuenzi UHURU WA TANZANIA na kuendelea kutunza Mazingira ya Nchi.
Halikadhalika Mh Sophia Kizigo amewapongeza Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika Shuhuli hiyo ya upandaji Miti.
Tutumie mda huu tulipotoka mpaka hapa tulipo,mambo yamebadilika na kuondoa baadhi ya mambo ili kudumisha Amani.
Lililofanyika lolote kwenye Nchi yetu ni matunda ya "Uhuru na tunatakiwa kuwa mabalozi kwa chochote kinachoonekan leo kitunze ili kiweze kutumika miaka ya mbele ijayo kwa faida ya watoto wetu."Amesema Dkt Kizigo.
Kauli Mbiu ya mwaka huu "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu"
Heri ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.