Acha Mazoe kwenye kituo chako cha kazi,jifunze ili uweze kukuwa kitaaluma hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilayani Mpwapwa Machi 10,2025.
Bw.Kaspa amewataka watumishi hao kuacha mazoea katika vituo vyao vya kazi na badala yake wafanye kazi kwa kujifunza ili waweze kukua kitaalama zaidi na kuweza kutoa matokeo mazuri ya utendaji kazi wako.
Akizungumza na watumishi hao amesema ni lazima utambue wajibu wako ukiwepo kazini na kuweza kutekeleza majukumu yako ipasavyo,hii itapelekea mtumishi kuweza kujiamini katika nafasi yake aliyokunayo na kuwaasa watumishi hao waache kutembelea cheo alichonacho kama mtumishi wa Serikali.
"Acha mazoea kwenye kazi,kila siku jifunze ili uweze kujuwa kitaaluma usizoee kazi,bosi wala kiongozi wako ila usimuogope"
"Tembea kifua Mbele kwa kujiamini unatosha kwa nafasi hiyo,ila usitembee na cheo chako kama mtumishi wa Serikali"amesema Gasper
Aidha amewataka Watumishi kuishi kwa upendo wakiwa kazini na kusisitiza suala la kufanya kazi kwa kushirikiana(team work)ili kuweza kufikia malengo ya kimkakati ya Halmashauri.
Halikadhalika alisema ni vizuri kwa watumishi kuwa na usiri katika kazi za Serikali na pia kuacha tabia ya kumuibia muajiri wake,ni wajibu wake kufika kazini,kuwepo na kuondoka kwa muda unaotakiwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.