Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe George O Fuime amefanya ziara ya kikazi leo Disemba 13,2024 na kukagua Miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa.
Wakati wa ziara yake hiyo amekagua Shule ya Sekondari Sijila inayoendelea kujengwa katika kata ya PwagaI, Shule ya Sekondari Simbachawene iliopo Kata ya Luhundwa kijiji cha Kitenge ambayo inaendelea na ujenzi zote zikiwa na gharama ya Shilingi milioni 544,225,626 kutoka SEQUIP pamoja na kukagua Daraja la mlatu liliopo Kata ya Mbuga kijiji cha Mbuga. lililojengwa kwa nguvu za Wananchi,fedha za Mfuko wa Jimbo pamoja na HalmashaurijumlaniShiling11,500,000.
Ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi imefanyika wilayani Mpwapwa katika kata mbali mbalii kwa lengo la kuangalia maendelea ya miradi hiyo na kuwahamasisha wasimamizi na mafundi wa miradi waweze kumaliza kwa wakati uliowekwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.