Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imefanya mnada wa kuuza Magari chakavu tisa (9), mnada huo umefanyika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Magari yaliyouzwa ni tisa yalifanyiwa tathimini kuwa na thamani ya fedha za kitanzania shilingi Milioni thelathini na moja laki tatu na elfu hamsini tu (Tsh 31,350,000) ila baada ya mnada kumalizika magari yote yaliuzwa kwa shilingi Milioni sabini na moja na laki nne tu (Tsh 71,400,000).
Aidha akitoa taarifa katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul M. Sweya amesema "kutokana na mnada wa uuzaji wa magari chakavu Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepata fedha mara mbili ya kiasi cha fedha iliyothaminiwa mwanzo". Hivyo halmashauri imesimamia vizuri mnada huo na kila mnunuzi amechukua gari lake.
Orodha ya Magari yaliyouzwa:-
Moja ya Gari lililonunuliwa likiwa limepakiwa katika Lori kwa ajili ya kusafirishwa.Magari chakavu yaliyopaki kwa ajili ya kupigwa mnada.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.