Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe S. Kebwe atoa Rai kwa Madiwani wote Nchini Kupewa Mafunzo Maalumu ya Komputa.
Ameyasema hayo leo tarehe tarehe 09.05.2017, wakati akifungua Rasmi Mafunzo Maalumu ya Uendeshaji na Utunzaji wa Kumbu kumbu za Vikao vya Mabaraza ya Madiwani kwa Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya zote nchini. Mafunzo hayo ya siku tano yanayoendeshwa na Wakufunzi kutoka katika Chuo cha Utumishi wa Umma, yanahusisha pia Makatibu Kamati wote Nchini yanafanyikamkoani Morogoro.
Amesema “Madiwani wafundishwe Matumizi ya Komputa ili kuweza kurahisisha upashanaji Habari na Taarifa muhimu hususani katika zama hizi za utandawazi, hatua itakayowezesha Wajumbe kupata taarifa muhimu za Vikao kwa wakati, lakini pia kupungua kwa gharama za uendeshaji wa Vikao” Hivyo ametoa wito kwa waandazi wa mafunzo hayo kuandaa mafunzo hayo maalumu.
Akitoa salamu za ukaribisho Mkuu wa Mkoa amewakaribisha Wakufunzi na Wakurufunzi Mkoani Morogoro huku akitoa wito wa kutumia fursa zilizopo katika kuwekeza hususani katika Sekta ya kilimo kwa kuwa Azimio la Serikali kuhamia Dodoma limetoa fursa kwa mkoa wa Morogoro kuwa ni wa kimkakati.
Ametoa wito pia kwa washiriki kuzingatia mafunzo ili waweze kuelewa na kupata maarifa yatakayo waongezea ufanisi wa kiutendaji huku akisisitiza kuwa Wenyeviti wanapaswa kusimamia taratibu za Vikao ili Vikao hivyo viweze kuendeshwa vizuri.
Vile vile Amewaasa Wenyeviti hao kusimamia suala la ukusanyaji wa mapato huku msisitizo ukiwa ni kwenye Matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato.
Washiriki wakiwa wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi, Leo Tarehe 09.05.2017 Mkoani Morogoro
Kupata Vitini Vya Mafunzo Fuata Linki Hii: http://www.mpwapwadc.go.tz/storage/app/uploads/public/591/ab3/db1/591ab3db1d3c1691441569.zip
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.