Mkurugenzi tendaji wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Mohamed A. Maje, amewaasa wananchi wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii ili waweze kutibiwa kwa urahisi pindi watakapougua.Ametoa wito huo katika huduma ya Kliniki Tembezi iliyotolewa hivi karibuni katika Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa ambapo wagonjwa zaidi ya 3000 walijitokeza kukutana na madaktari bingwa wa Mkoa wa Dodoma ambao wametoa huduma za kitabibu kwa magonjwa mbali mbali. Amesema kuwa Mfuko huo ni mkombozi wa wananchi wa hali ya chini kwa kuwa unawawezesha wanafamilia sita kutibiwa kwa kiasi cha Tsh 10,000.00. Wito huo umetolewa kutokana na changamoto ambayo wananchi wasiokuwa na Bima wamekuwa wakiipata ikiwa ni pamoja na kulipa Malipo ya papo kwa papo ambayo huwalazimu wagonjwa kulipa kila wanapotibiwa.
Msululu wa wagonjwa waliojitokeza kupewa tiba katika huduma ya Kliniki Tembezi iliyofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa Kuanzia tarehe 13.03.2017-19.03.2017
Kutoka kulia ni Bw. Mohamed A. Maje Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Mpwapwa akiwa na Katibu Tawala (W) Ndugu Athanasia Kabuyanja wakitoka kuwajulia hali wagonjwa
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.