Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kiwilaya yamefanyika Kijiji cha Idilo kata ya Mazae leo tarehe 08 Machi,2028 na Kuhudhuriwa na Diwani wa kata hiyo Mhe.Willium Madanya ambae ndio Mgeni Rasmi.
Mhe.Madanya amewapongeza wamama wote duniani kwa uwezo mkubwa waliobarikiwa na Mungu kuweza kuvumilia vitu vingi kwa wakati mmoja na kuweza kupambana katika shuhuli tofauti zikiwemo za kiuwonhozi na kutoa mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa takribani viongozi wote wanaotuzunguka kiuwongozi ni wanawake.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanaenda Sambamba na Kauli Mbiu isemayo
"Wanawake na Wasichana 2025,tuimarishe Haki,Usawa na Uwezeshaji"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.