Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mh George O Fuime ameongoza kikao cha mrejesho wa zoezi la uandaji mpango shirikishi wa matumizi ya ardhi misitu katika vijiji vya Lufusi,Mbuga,Igului,kizi na Galigali kutoka kampuni ya Compassion Cabon.
Ndg Laurent kutoka Shirika la mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu ameelezea namna ya hatua zilivyofanyika kutekeleza mipango hiyo kwa kufuata na kuzingatia Sheria,Sera na miongozo inayosimamia sekta za ardhi na misitu.
Pia amesema wametumia njia ya usimamizi shirikishi kwa kufanya mikutano ya viyongoji na mkutano mkuu wa vijiji ili zoezi liweze kuendele na baadae halmashauri ya kijiji ilikaa na kutoa mapendekezo yao na kumalizia na mkutano mkuu kwa kupitisha makubaliano hayo kwa pamoja.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.