Mafunzo ya waandikishaji wa daftari la wapiga kura yamefanyika Leo Octoba 8,2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mpwapwa.
Katika Mafunzo hayo yaliyotembelewa na waratibu wa kamati ya Uchaguzi kutoa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kukagua uendeshaji wa semina mbali mbali zinazoendelea Mkoa wa Dodoma
Bi Coletha amewataka na kuwasisitiza waandikishaji wa daftari la wapiga kura kuzingatia muda wa kuanza kwa zoezi hilo ili waweze kufikia lengo,kufanya uhamasishaji, kutoa taarifa kwa wakati pindi tu wanapomaliza zoezi la uwandikishaji kwa kila siku na maadili wanapokuwa vituo vya kazi na hata kwa jamii inayowazunguka ili kuweza kuepukana na mambo yasifaa.
Lengo la semina hiyo kwa waandikishaji wa daftari la wapiga kura ni kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mzuri bila ya kuharibu zoezi hilo
Zoezi la Uandikishaji wa wapiga kura litaanza tarehe 11 hadi 20 Octoba kwa Tanzania nzima.
#UchaguziwaSerikalizaMitaa2
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.