LIC (Local Investment Climate Project) ni mradi unaofadhili miradi mbalimbali ya uwekezaji katika sekta binafsi na umma. Pia hutoa misaada ya ushauri katika miradi ya uwekezaji ili kuwezesha miradi kuwa ya kudumu, endelevu na iwe darasa kwa wawekezaji wengine.
Mafunzo hayo yametolewa na wataalam wawili toka ofisi za LIC mkoani Dodoma kwa wakuu wa Idara, Vitengo na wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpwapwa. Mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na jinsi ya kuandaa Andiko la Biashara ili kuweza kupata ufadhili toka LIC au kwa wafadhili wengine. Aidha, wataalam hao toka LIC wamefundisha jinsi ya kufanya tafiti za masoko, kanuni za uwekezaji, kuandaa mpango wa biashara, kutambua viatarishi vya uwekezaji na kuthibiti athari za mazingira zinazotokana na uwekezaji.
Mwezeshaji wa LIC akitoa mafunzo kwa Washiriki.
Washiriki Wakifuatilia Wafunzo kwa Umakini mkubwa
Mwezeshaji Akifafanua Jambo katika Mafunzo hayo.
Kwa maelezo zaidi pakua nyaraka hapa chini:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.