MTAKUWWA ni Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. Mpango huu unatekelezwa nchini Tanzania kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2021/22, ambao upo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Wajumbe wa Kamati ya Wilaya ya MTAKUWWA wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji uliopo Wilayani Mpwapwa kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 Aprili hadi 23 Aprili 2018 na timu ya wataalam toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto.
Pamoja na kufundishwa mbinu mbalimbali za kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto, wataalam hao wamefundisha maeneo mkuu manane ya kuzingatia ili kupambana na ukatili huo kama yafuatayo.
1. Kuimarisha uchumi wa kaya
2. Mila na desturi.
3. Mazingira Salama kwa Wanawake na watoto.
4. Malezi, kuimarisha mahusino na kiziwezesha familia
5. Utekelezaji na usimamizi wa sheria
6. Utoaji wa huduma kwa waathirika wa ukatili
7. Mazingira salama shuleni na stadi za maisha.
8. Uratibu, ufuatiliaji na tathmini.
Mwezeshaji wa Mafunzo toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akifafanua jambo
Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA wa Wilaya Wakifuatilia Mafunzo kwa Umakini.
Kwa habari zaidi pakua taarifa hapa chini:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.