Vikao hivyo vilianza kwa kumkumbuka aliyekuwa Mh. Diwani wa Kata ya Wangi kwa kusimama na kunyamaza kimya kwa muda wa dakika tano, mheshimiwa huyo aliyefariki kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu. Vile vile vikao hivyo vya Mabaraza ya Kata vilianza kwa Waheshimiwa Madiwani kutoka kila kata kuwasilisha taarifa za Maendeleo, mikakati na shughuli zilizofanyika katika kata yake. Kila Mh. Diwani alipata fursa ya Kuwasilisha taarifa ya kata yake ambapo Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa ina jumla ya kata 33.
Mh. diwani akiwasilisha taarifa ya kata yake
Wakuu wa idara na wataalam mbalimbali wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa za kila kata.
Watendaji wa kata zote 33 za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa za kila kata.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.