Kamati ya Fedha Uongozi na Mpango (FUM) ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikiongozwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Fuime imefaanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi, sekondari pamoja na ujenzi wa vituo vya afya. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Zahanati ya Mgoma kata ya Godegode, Shule ya Msingi Pwaga, Shule ya Msingi Munguwi, Zahanati ya Munguwi, Shule ya MSingi Njiapanda, Zahanati ya Singhonali, Shule ya Sekondari Ikuyu, Kituo cha Afya Mtera, Kituo cha Afya Chipogoro, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Chitemo, Zahanati ya Chamanda, Shule ya Sekondari Chipogoro, Zahanati ya Mzase na Zahanati ya Chaludewa.
Aidha baadaya kukagua miradi yote FUM imetoa pongezi kwa miradi iliyokamilika na kufanya vizuri kama Ujenzi wa madarasa shule yaMsingi Pwaga, Ujenzi wa Mdarasa mawili ya Shule ya Msingi Kidenge, Ujenzi wa Madarasa ya Shule ya Sekondari Ikuyu pamoja na kituo cha afya Chipogoro.
Vile vile Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Fuime amewataka mafundi wote wanaojenga majengo ya maabara ya Shule ya Sekondari ya Chipogoro Kumalizia kazi ya mdirisha, na kituo cha afya Mtera kurekebisha mirango na madirisha.
Mwisho wajumbe wa FUM wamemtaka Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Cosmas Ngalula kutembelea, kukagua na kutoa ushauri katika ujenzi wa miradi mbalimbali katika halmashauri.
Wajumbe wa FUM wakikagua Kituo cha Afya Chipogoro (Kulia Mhe. George Fume, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa)
Wajumbe wa FUM wakikagua Madara mawili yaliyojengwa EP4R katika Shule ya Sekondari Ikuyu.
Wajumbe wa FUM wakikagua Kituo cha Afya Mtera (Hili ni jengo la Kuhifadhia Maiti)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.