Mkurugenzi wa Idara ya Afya,lishe na ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais_TAMISEMI,Dkt. Rashid Mfaume amefanya ziara ya kikazi Febuari 28,2025 katika Wilaya ya Mpwapwa na kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinapima ardhi za Zahati,vituo vya Afya na Hospital zote nchini ili kupata hati miliki za maeneo hayo.
Dkt.Mfaume ametoa ushauri huo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa jamii katika Mkoa wa Dodoma wilayani Mpwapwa alipotembelea kituo cha Afya Kibakwe.
"Nilazima tupime maeneo yetu tuweke mipaka rasmi,kuhakikisha yanakuwa na hati miliki ili kuzuia uvamizi" amesema Dkt.Mfaume
Ameongezea kuwa kasi ya ukuaji wa Mji inasababisha watu kuhamia karibu na vituo vya huduma,hivyo upimaji wa maeneo hayo utasaidiakulinda miundombinu ya Afya.
Halikadhalika amewakumbusha watumishi wa Afya kuandaa taarifa usahihi na zenye uhalisia kwani Serikali zinazitengemea kwa ajili ya kupanga mipango na usimamizi wa huduma kwa Wananchi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.