Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally amefanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya kimaemdeleo inayoendelea kujengwa katika Halmashaùri yake Julai 11,2025 akiambatana na wakuu wa idara na vitengo.
Wakati wa ziara yake hiyo amekagua miradi mbali mbali ikiwemo
Ujenzi wa bweni la wafunzi katika Shule ya Sekondari Berege likiwa na gharama ya Sh
125,000,000.00 hadi kukamilika.
Darasa moja lilogharamu kiasi cha Sh 23,000,000 na Ujengwaji wa jiko la kupikia wanafunzi ambalo litagharimu kiasi cha Sh.40,000,000 hadi kumaliza kwake
Pia amekagua Ujenzi wa Nyumba ya Mganga 3 in 1 inayoendelewa kujengwa katika Zahanati ya Mima itakayogharimu Sh 110,000,000 na ununuzi wa dawa
katika kituo cha Mima zenye thamani ya Sh 14,372,000.00.
Halikadhalika ziara huyo iliendelea katika Shule ya Msingi Seluka iliopo kata ya Chipogoro kwa lengo ĺa kufanya tathmini ya ukarabati wa Shule hiyo juu ya miundo mbinu iliyochakaa.
Pia ziara iliendelea katika kituo cha afya Rudi na kutembelea mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya afya ikiwemo kichomea taka na vyoo vyenye gharama ya Sh.87,000,000 na kukagua ununuzi wa Genereta uliogharimu 137,000,000 pamoja na kujengewa kwake
Na mwisho alikaua ujenzi wa Maabara katika kituo cha afya kibakwe chenye gharama ya Sh 94,000,000 hadi kukamilika kwake.
Bi Mwanahamisi amewataka wasimamizi wa mirafi hiyo pamoja na mafundi waengeze kasi ya utendaji kazi wao ili miradi iweze kumaliza kwa wakati na pindi wanapotokewa na changamoto yoyote wasisite kusema ili waweze kutatua changamoto hizo kwa pamoja.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.