....Baraza la biashara la wilaya ya Mpwapwa limeazimia kuwa Soko la wafanyabiashara wadogo wadogo la Mji Mpya lifunguliwe mara moja ili kuwapunguzia adha wafanyabiashara wadogo wadogo ikiwa ni pamoja na kurasimisha biashara zao na kuiongezea Halmashauri Mapato. Hayo yameafikiwa katika kikao cha kawaida cha Baraza la Biashara la Wilaya leo tarehe 31.03.2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri. Ujenzi wa Soko la Mji Mpya ulianza mwaka 2008 na kukamilika mwaka 2014 baada ya kuibuliwa na wananchi wa mjimpya Mpwapwa. Ni Mradi uliojengwa kwa Nguvu za wananchi na ufadhiri wa TASAF II (kiasi cha 46,152,927.28). Akitoa ufafanuzi Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa Ndugu Seleman Mtinangi amesema kuwa Soko hilo halijafunguliwa kwakuwa ujenzi wa miundombinu bado haujakamilika na kuna mikakati mbali mbali iliyopo ya kuhakikisha kuwa soko hilo linafunguliwa ikiwa ni pamoja na kuomba fedha katika taasisi ya LIC ili kuweza kumalizia miundo mbinu ya Choo, Umeme na maji kiasi cha sh 25,408,878.00. Hata hivyo Halmashauri imekwishatoa kiasi cha Tsh 10,000,000.00 ambayo imeanza kutumika kurekebisha miundombinu ya choo. Aidha amewatoa wasiwasi wajumbe wa Baraza hilo kuwa soko litafunguliwa mara baada ya choo hicho kurekebishwa.
Wajumbe wa Baraza la Biashara wakijadiliana katika kikao cha Baraza la Biashara katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Wajumbe wa Baraza la Biashara wakijadiliana katika kikao cha Baraza la Biashara katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.