Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpwapwa lafanya kikao cha pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mpwapwa, hii ni kutokana na jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Mh. Jabir Shekimweri za kuhakikisha Baraza la Biashara linashirikisha wadau na wafanyabiashara toka kila kona ya Wilaya ya Mpwapwa ili kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo yanayohusu biashara na fursa zake.
Pia katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya huyo amesema, hili ni baraza la pila la wafanyabiashara, la kwanza lilivunjwa kwasababu halikuwa na sura ya Wilaya kwa kuwa lilishirikisha wadau na wafanyabiashara (wadau wa sekta ya umma na binafsi) wa mjini, wengi wao walikuwa wadau toka sekta ya umma, ila kwa baraza hili la sasa limehusisha wadau karibu kutoka kila kona za Wilaya.
Pia washiriki hasa wafanyabiashara wa sekta binafsi wamelalamikia kutofikiwa na elimu ya biashara hususani katika mashuala ya kodi na jinsi zinavyotozwa. Hata hivyo Afisa Biashara wa Wilaya Bw. Bilton Otto alisema walishatoa elimu karibu maeneo yote ya wilaya na hivyo atapanua wigo wa kuwafikia wadau wengi zaidi haya maeneo ya Vijijni.
Wajumbe na waalikwa wakiwa katika kikao cha pamoja cha Baraza la Biashara na Madiwani.
Washiriki wa kikao cha Baraza la Biashara na Baraza la Madiwani wakifuatilia mjadala.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akihutubia Baraza la Biashara katika kikao cha baraza hilo na Madiwani
Kwa taarifa zaidi pakuwa hapa chini:-
2.KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA NA BARAZA LA MADIWANI.pdf
3.MIRADI ILIYOFADHILIWA LIC.pdf
4.TAARIFA YA BARAZA LA BIASHARA.pdf
5.TAARIFA YA MAENDELEO YA BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA MPWAPWA KUANZIA 2015-2018.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.