Tuesday 21st, January 2025
@Mpwapwa
Serikali imeobwa kuweka mkakati maalum wa kudhibiti wimbi la uwizi wa punda unaotokana na kukithiri kwa uhitaji wa ngozi ya Punda, kutokana na mnyama huyu kuwa katika hatari kubwa ya kutoweka nchini na hivyo kusabisha kuongezaka kwa wimbi la umaskini kwa jamii nyingi za vijijini zinazo mtegemea mnyama huyu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kubeba mizigo..
Matukio ya uwizi wa punda yamekuwa yakiongeeka kila kukicha sehemu mbalimbali za wilaya ya Mpwapwa na mkoa mzima wa Dodoma. Katika Tukio lililotokea katika kijiji Mzase kata ya Berege wilayani hapa punda watano wamekutwa wameibwa na kuchunwa ngozi huku mizoga yao ikiwa ametelekezwa porini.
Mmoja wa wanakijiji hicho bwana Naftari Asheri amesema kuwa endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa za kuweza kuokoa wizi wa punda kuna uwezekano mkubwa wa wanyama hao kutoweka na na hivyo kusababisha ongezekao la umaskini sehemu za vijijini kulingana na umuhimu wa mnyama huyo katika maisha ya Mtanzania. Aidha Bwana Naftari alisema kuwa lazima serikali iweke mkakati madhubuti wa kukabiliana na changamoto ya kumuokoa mnyama huyo ambae siku za hivi karibuni amekuwa akiwindwa zaidi kuliko mnyama yoyote yule.
Mkurugenzi wa shirika la TAWESO Dkt. Kahema alisema kuwa kutokana na kuzidi kushamili kwa biashara hii ya ngozi za punda katika jamii kunatishia wanyama hawa kuzidi kupungua siku hadi siku na kusababisha kupungua kwa nguvu kazi ya mfugaji wa punda kila kukicha. Aidha Dkt Kahema alisema kutokana na utafiti uliofanywa na shirika hilo imebaini kuwa kila siku punda zaidi ya mia moja wanauwawa kila siku kwa kuchinjwa kama kitoweo au kwa ajili ya kuuza ngozi yake katika viwanda vya wachina vilivyoko Dodoma na Shinyanga na katika jamii. Alisema kuwa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa ndani ya miaka mitatau mbeleni taifa litakuwa halina mnyama kazi kama punda kutokana na biasahara ya ngozi yake kushika kasi sana katika bara la Asia hasa nchini China.
Hata hivyo Dkt Kahema alisema kuwa kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na punda wasio zidi laki tano nchi nzima lakini uwiano wa uzalishaji na uchinjaji wa Punda kwa siku haviendani na kutishia mnyama huyo kutoweka kabisa katika jamii. Alidai kuwa Punda amekuwa akifanya kazi za kila siku za mwananchi wa hali ya chini kijijini hivyo mnyama huyo akipotea basi wimbi la umaskini litaongezeka hapa nchini. “ Unajua kwa sasa punda mzima anauzwa kwa shilingi laki mbili wakati kwa mwaka punda anafanya kazi za zaidi ya milioni tano kwa mkulima kama kulima, kuchota maji, kubeba mizigo na shughuli zote za kila siku kwa mkulima” aliongea Dkt Kahema.
Alisema kutokana na ugumu wa maisha ya mnyama huyu uzalishaji wake kwa mwaka umekuwa wa shida ambapo punda hubeba mimba kwa miezi 12 na huingia joto mara baada ya miaka mitatu hivyo huzalishaji wake umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na upoteaji wake katika jamii. Katika kipindi cha miezi sita punda zaidi ya 27 walichunwa ngozi na mizoga yao kutelekezwa, matukio hayo yalilipotiwa katika kituo cha polisi na kesi zikiwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali hapa wilayani hapa
Mizoga ya punda ikiwa imetelekezwa porini katika kijiji cha Mazase kata ya Berege
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.