Friday 10th, January 2025
@Wilaya ya Mpwapwa
Mkoa wa Dodoma mnamo tarehe 30 Julai 2018 unatarajia kuupokea Mwenye wa Uhuru kimkoa katika Wilaya ya Mpwapwa kata ya Lumuma ukitokea Mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilosa. Katika mapokezi ya mwenge huo wanatarajiwa kuhudhuria wakuu wa mikoa wote wawili wa Mkoa wa Morogoro na Dodoma, wakuu wa Wilaya zote za Morogoro na Dodoma, Wakurugenzi wote wa Morogoro na Dodoma, makatibu tawala wa wilaya zote Morogoro na Dodoma, na wageni wengine waalikwa katika sherehe hizi, pamoja na wananchi wote kwa ujumla.
Kwa upande wa Wilaya ya Mpwapwa Mwenge huo unatarajiwa kutembelea miradi ifuatayo: Shule ya Awali na Msingi ya Franco Badian iliyopo kata Lumuma, Kituo cha Afya cha Pwaga kilichopo kata ya Pwaga, Kituo cha Wanyama kazi Kibakwe kilichopo kata ya Kibakwe, Barabara ya Kidenge - Lufu, Mradi wa Maji wa Luhundwa, The Mother land shule ya English Medium iliyopo kata ya Mpwapwa Mjini katika Kijiji cha Ilolo na Kiwanda cha Kukamua alizeti, kusaga na kudindika unga wa mahindi.
Eneo la mkesha wa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwa Ilolo ambapo patakuwa na shughuli mbalimbali za maonesho kama vile shughuli za kupambana na rushwa (TAKUKURU), shughuli za kupambana na madawa ya kulevya, shughuli za upimaji wa virus vya ukimwi (VVU) kwa hiari na malaria, utambulisho, kusoma risala na ujumbe wa mwenge. Pia katika eneo hilo la mkesha kutakuwa na burudani mbalimbali kama vile muziki, vikundi vya ngoma, skauti, vikundi vya salakasi, vikundi vya maigizo, kwaya, ngonjera na wacheza shoo (Stage Show).
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu 2018 ni "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA, WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
Kwa ujumla katika wilaya ya Mpwapwa mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa takribani kilometa 148 mpaka kufika Igunga wilayani Kongwa ambalo litakuwa eneo la makabidhiano.
Wananchi wote mjitokeze kuupokea na kuusherekea Mwenge wa Uhuru, Nyote mnakaribishwa.
.......MWENGE HOYEEEEEEEEEEEEEEEE..........................
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.