Tuesday 21st, January 2025
@SHULE YA SEKONDARI NGHAMBI
Mwenge wa Uhuru umefika Wilayani Mpwapwa na kukimbizwa takribani kilometa 191.1, kiongozi wa mbio za Mwenge Bw Abdallah Shaib Kaim ametembelea na kukagua vyumba 9 vya madarasa,pia amezindua klabu ya lishe,klabu ya wapinga rushwa TAKUSKA na kutembelea kitalu cha miti na miti iliyopandwa,vilevile ametembelea na kukagua mradi wa vijana na mshikamano unaojishuhulisha na utengenezaji wa bidhaa za GYPSUM.
Halikadhalika ameshiriki zoezi la upandaji miti katika Chuo cha Uwalimu Mpwapwa ,na kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa maboresho ya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.Pia aliweka Jiwe la Msingi katika mradi wa Maji Lupeta na mwisho ameweka Jiwe la Msingi barabara ya Lami Kibakwe yenye KM 1.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.