Friday 18th, July 2025
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Ndg Erick Ntikahela ambae ni Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Ufuatiliaji na Tathimini ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kupata Hati Safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika Juni 18, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Ndg Ntikahela . amesema mafanikio hayo ni ushahidi wa usimamizi mzuri wa fedha za umma, uwajibikaji na ufuatiliaji thabiti wa matumizi ya serikali.
“Kupata Hati Safi si jambo dogo, ni matokeo ya kazi kubwa. Nawaomba viongozi na wataalam muendelee kulinda heshima hii kwa kuhakikisha hoja zisizokuwa za lazima hazijitokezi tena." amesisitiza Ndg Ntikahela
Pia amesisitiza ili kuepukana na changamoto za kuwa na hoja nyingi halmashauri ikakikishe kamati ya fedha inayokutana kila mwezi iwe na ajenda ya kudumu kujadili mwenendo wa ujibuji wa hoja za ukaguzi wa ndani na nje ili kupunguza hoja za halmashauri.
Halikadhalika amesisitiza usimamizi madhubuti ya ruzuku za fedha za wanafunzi ili malengo ya Serikali yaweze kutimia.
Naye Mkuu wa Wilaya Mh Dkt Sophia kizigo amelipongeza baraza la Madiwani kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na mafanikio makubwa waliyoyapata katika kata zao.
"Baraza hili ndio baraza pekee lilokusanya mapato kwa 112%mwaka jana ikiwa mwaka huu limefikia 102.8 na ndio baraza pekee kila kata ndani ya Wilaya ya Mpwapwa imepata Serikali"amesema Dkt Kizigo.
CAG hutoa aina nne za hati baada ya ukaguzi, ambazo ni: Hati Inayoridhisha (Hati Safi), Hati Yenye Mashaka, Hati Isiyoridhisha, na Kutotoa Hati (Hati Mbaya). Hati Safi hutolewa pale ambapo Mkaguzi anaridhika kuwa taarifa za kifedha zimetayarishwa kwa usahihi na kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.