Tuesday 21st, January 2025
@Mpwapwa Shule ya Sekondari
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo wamepatiwa mafunzo ya Mifumo ya Mipango na Bajeti (PLANREP) pamoja na Mfumo wa Kihasibu wa katika Ngazi ya Kutolea Huduma (FFARS). Akifungua mafunzo haya Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Pius Sayai kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa bajeti ya mwaka huu ifuate mwongozo wa bajeti wa mwaka 2019/2020 ili kuandaa bajeti yenye kutekelezeka. Pia Ndug. Sayai ame sisitiza kuwa mafunzo haya yana madhumuni ya kuwajengea uelewa washiriki, kupata na bajeti inayotekelezeka na kupunguza hoja za mkaguzi kwa kufuata vifungu husika katika kupanga bajeti, kuelewa miongozo na maelekezo ya Serikali.
Mafunzo haya yamehudhuria na wakuu wa idara na vitengo wote pamoja na baadhi ya watumishi wa chini yao. Pia walimu wakuu na wahasibu wa shule za msingi na sekondari wamepatiwa mafunzo haya toka kwa Ndug. Bendera mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Afisa Utumishi Ndug. Pius Sayai (katikati) akifungua mafunzo ya FFARS na PLANREP kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri katika Ukumbi wa Mpwapwa Shule ya Sekondari
Wakuu wa idara wakiwa katika mafunzo ya FFARS na PLANREP katika Ukumbi wa Mpwapwa Shule ya Sekondari
Wakuu wa idara wakiwa katika mafunzo ya FFARS na PLANREP katika Ukumbi wa Mpwapwa Shule ya Sekondari
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.