Tuesday 21st, January 2025
@Shule ya Msingi Mtejeta
Siku ya Mtoto Afrika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana. Katika siku hii watoto wote wa Mpwapwa wamekaribishwa na kuungana na wazazi wao katika kusherekea siku hiyo. Mgeni rasmi katika sherehe hii ni Dr. Emmanuel Saro ambaye pia ni Afisa usafi na Mazingira wa Wilaya ya Mpwapwa.
Aidha waheshimiwa madiwani, Wakuu wa Idara, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi na viongozi wa mashirika mbalimbali wamekaribishwa katika sherehe hii.
Mgeni rasmi (wa kwanza kutoka kulia) akisikiliza kwa makini taarifa ya wilaya kuhusu huduma mbalimbali za watoto wilayani Mpwapwa.
Mgeni rasmi (wa kwanza kutoka kushoto katika meza kuu) akisikiliza kwa makini taarifa ya wilaya kuhusu huduma mbalimbali za watoto wilayani Mpwapwa.
Watoto wilayani Mpwapwa wakiwa katika Mstari tayari kwa kupata chakula kulichoandaliwa kwenye sherehe hiyo.
Kupata Taarifa ya Wilaya kuhusu watoto na Hotuba ya Mgeni rasmi, Bofya viungasnishi hapo chini.
Hotuba ya Mgeni rasmi Siku ya Mtoto Afrika.pdf
Taarifa ya Wilaya kuhusu huduma za Watoto Wilayani Mpwapwa.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.