Saturday 21st, December 2024
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Baraza la Madiwani robo ya tatu limefanyika Agosti 5,2024 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kutolewa taarifa za Utekelezaji kutoka kwenye kamati zote za Madiwani.
Halikadhalika,kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Erick Anthony ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa ukusanyi mzuri wa mapato kwa 112% na kuweza kuvuka lengo walilojiweka na kuwataka waendelee na kasi hiyohiyo ya ukusanyi huo wa mapato,pia amelitaka baraza kusimamia suala la Maadili kwa watoto ili watoto wakue katika misingi ya maadili mema,hata hivyo amesisitiza usimamizi mzuri wa Miradi ya Kimaendeleo na kuhakikisha mradi unakwisha kwa wakati bila kuacha kovu wala deni kwa mzabuni na mafundi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.George O.Fuime ametoa agizo la kumaliziwa hoja zilizobakia pamoja na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji kufanya mpango wa kuhakikisha anapunguza madeni ya watumishi wanaodai.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.