Saturday 22nd, February 2025
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Mapema leo hii umefanyika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauti Mhe.George O. Fuime ukiwa na lengo la kujadili Makisio ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mpwapwa na Baraza hilo kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwa inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Tshs.44,212,778,238.00 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Halmashauri.
Ikumbukwe kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa iliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi 44,116,778,238.00 kwa ajili ya uendeshaji wa halmashauri na utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.