Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kutekeleza miradi inayotekelezwa katika maeneo yao. Ameyasema hayo hivi karibuni katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.Mhe. Nghwenzi amesisitiza kuwa fedha zote za miradi zinazopelekwa katika vijiji, uongozi wa Kijiji, Kamati ya Ujenzi, na Wananchi washirikiane ili miradi hiyo iweze kumalizika kwa wakati na kwa Ufanisi. Aidha amewataka viongozi kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza Maendeleo badala ya kukwamisha kutokana na masilahi binafsi.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika Kijiji cha Kidenge. Ujenzi huu upo katika hatua ya umwagaji wa Jamvi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.