.........Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe, George Simbachawene, ametoa agizo hilo leo wakati akizindua rasmi Tovuti za Mikoa na Halmashauri ambapo ametaka Maafisa habari wawezeshwe vitendea kazi hususani kamera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo ya kuhakikisha kuwa Tovuti za Mikoa na Wilaya zinakuwa Majokofu ya kuhifadhia taarifa sahihi na matukio muhimu wakati wote. Waziri amewaagiza wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa sekretarieti za Mikoa zinafanikisha utekelezaji wa agizo hilo na kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa watakaoshindwa kutekeleza huku akiwataka maafisa habari kuhakikisha kuwa Tovuti zinahuishwa kila wakati kwa kuwa na taarifa mpya na matukio mapya.
Maafisa Tehama na Habari waliotengeneza Tovuti
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.