Watendaji Kata wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Januari 29,2026 wamepatiwa mafunzo ya E_Mrejesho yakiwa na Lengo la kuwapa elimu zaid juu ya usikilizaji Kero na Malalamika kwa Wananchi wao.
Mafunzo hayo yaliyotelewa na Afisa Malalamiko Mkoa Ndg Gwamaka Mlagila,amewataka watendaji Kata hao kuishi vizuri na Wananchi wao na kuwatatulia matatizo yao bila kufikishana ngazi za juu..
Pia amewasisitiza kutumia njia za mawasiliano tofauti ili wananchi waweze kuzitumia katika kufikisha malalamiko au kero zao zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku,na kutoa mfano wa njia hizo ikiwemo Simu,mfumo wa e_mrejesho,mikutano pamoja na sanduku la maoni.
Hata hivyo hakusita kueleza wajibu wa kushuhulikia malalamiko ni pamoja na mikutano wa Kijiji e_mrejesho iingie kwenye agenda ambapo kero na malalakiko yote yatolewe utatuzi.
Halkadhalika,ndg Mlagila amewata kutumiza majukumu yao kwa kufuata yale yote ya Msingiyaliyozungumzwa yakafanyiwe kazi.
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika katika Ukumbi wa Biashara wilayani Mpwapwa.







Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.