Uongozi wa Afya kutoka Mkoa wa Dodoma umetoa mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya Mpwapwa yanayohusiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya NHIF Mei 08,2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwaletea Wananchi uelewa wa bima ya afya kwa wote na umuhimu wa bima ya Afya katika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita na kuhakikisha kila Mwananchi anaweza kupata huduma za afya.
Bima ya Afya kwa wote imeanzishwa chini ya sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Na. 23 ya 2023,iliyoanza rasmi tarehe 1/12/2024 ikifuatiwa na kanuni zake zilizotangazwa na gazeti la serikali Na. 70A/2024 zilizoanza kutumika mnamo tarehe 16/08/2024.
Sheria imelenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya kwa kuanzisha Mamlaka itakayosimamia na kuratibu shughuli za bima ya afya Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) ambapo chini ya TIRA huduma za bima kutoka skimu za bima ya afya zitaweza kuratibiwa kwa utaratibu maalumu utakaowekwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.