Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango (FUM)ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh George Fuime Imefanya ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika maeneo tofauti wilayani Mpwapwa Oktoba 21,2024 na kukagua Mradi wa Shule ya Sekondari Sijila iliopo kata ya Pwaga wenye thamani ya Sh. 544,225,626 kutoka SEQUIP.
Shule ya Sekondari Simbachawene iliopo kata ya Luhundwa wenye thamani ya Sh. 544,225,626 nao kutoka SEQUIP. Shule zote zipo katika Hatua ya awali ya Msingi.
Pia ilitembelea Zahanati ya Mangui kutoka kata ya Pwaga, zahanati ya Mpwanila iliopo kata ya Luhundwa, Zahanati ya Ng'ambi iliopo kata ya Ng'ambi na Zahanati ya kisokwe kutoka kata ya Mazae,na kwa kila mradi umegharimu kiasi cha Sh. 50,000,000. katika zahati zote kamati ilikagua Sehemu ya kunawia mikono, matundu mawaili ya vyoo kwa ajili ya wahudumu wa Afya na Kichomea taka kimoja,
Halukadhalika kamati imemalizia ziara take kWa kukagua Mradi wa Lambo wenye thamani ya Sh. 208,340,000 na Jengo LA kuhifadhia Dhana za Kilimo lenye gharama ya Sh. 55,623.000 yote kutoka EBBAR Iliyoopo kata ya Ng'ambi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.