Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Dkt Sophia Mfaume Kizigo leo Agosti 14,2024 ameendelea na ziara yake yakusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua na kutembelea Miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika kata ya Mlembule,Matomondo na Lupeta
Katika Ziara yake hiyo iliyoanzia Kata ya Mlembule ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya,na Mtomondo amekagua mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata na kumalizia na mkutano wa hadhara kwa kila kijiji kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi na kuzitolea utatuzi.
Mhe.Kizigo ametoa maagizo mbali mbali kwa viongozi wa kila kijiji kwa kuhakikisha wanafanya mikutano na wananchi wao na kuwajuza mapato na matumizi yanayotumika ndani ya vijiji vyao,pia kupimwa kwa matirio ya vifaa yaliyotumika katika ujenzi,mbali na hayo amewakumbusha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchaguz viongozi wanaofaa.
"KERO YAKO WAJIBU WANGU"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.