Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Dkt Sophia Mfaume Kizigo leo Agosti 13,2024 ameendelea ziara yake yakusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua na kutembelea Miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika kata ya Kimaghai,Ving'awe na Mpwapwa mjini.
Katika Ziara yake hiyo iliyoanzia Kata ya Kimaghai Mhe.Kizigo amegua marekebisho ya vyoo pamoja na vyumba vya maabara katika S hule ya Sekondari KImaghai A,pia amekagua mradi wa madarasa mawili ya Shule Shikizi Ving'awe na katika Shule ya Sekondari Ving'awe amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita amabyo yapo katika hatiua ya awali,na katika kata ya Mpwapwa mjini ametembelea mradi wa vumba vya madarasa mawili pamoja na ujenzi wa matundu sita ya vyoo katika Shule ya Mount Igovu,pamoja na hayo Mhe.Kizigo amefanya mkutano wa hadhara kwa kila kijiji na kusikiliza kero za Wanachi na kuzitolea utatuzi.
Mhe.Kizigo ametoa maagizo mbali mbali kwa viongozi wa kila kijiji kwa kuhakikisha wanafanya mikututano na wananchi wao na kuwajuza mapato na matumizi yanayotumika ndani ya vijiji vyao,pia kupimwa kwa matirio ya vifaa yaliyotumika katika ujenzi,mbali na hayo amewakumbusha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchaguz viongozi wanaofaa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.