Tuesday 21st, January 2025
@Mpwapwa
BAADHI yawafugaji katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameingia hasara kwa kupoteza mifugo yao aina ya nguruwe kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa nguruwe ujulikanao kama African swine fever. Wakiongea na mwanahabari wetu kwa nyakati tofauti mmoja wa wafugaji Bi Tabitha Simbeye alisema tangu ugonjwa huo uzuke wafugaji wengi wamepoteza nguruwe wengi na hivyo kuwasababishia hasara kubwa. Tabitha alisema katika zizi lake kulikuwa na nguruwe sita wote walikubwa na ugonjwa baadhi alifanikiwa kuwauza kwa bei ya hasara na wengine walikufa na kuwazika.
Alisema nguruwe wengi wameathiriwa na ugonjwa huo, ambapo alisema Nguruwe wakipatwa na ugonjwa huo hutetemeka, kukosa nguvu na kushidwa kutembea. Aidha mmoja wa watafiti wa mifugo kutoka katika Tasisi ya utafiti wa mifugo TARILI Mpwapwa ambae jina lake hakutaka liiandikwe alisema kuwa ugonjwa huu hutokea kwa msimu, na unasababishwa na virusi, hivyo ni ngumu kutibika wala kukinga. Mtafiti huyo alisema ili kuweza kudhibiti ugonjwa huo ni kupiga karantine za shughuli zote za mifugo ikiwemo minada na shughuli zingine zote ili kuzuia ugonjwa huo kuenea kwa wingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri yaWilaya ya Mpwapwa bwana Mohamed Maje alikili kuzuka kwa ugonjwa huo wilayani kwake. Alieleza kuwa ugonjwa huo uliotekea mkoani Morogoro na alisema tayari alishatoa maelekezo kwa maofisa mifugo ngazi ya kata na vijiji ikiwemo kusitisha shughuli zote zinazohusiana na uchinjaji, uuzaji na na usafirishaji wa mazao yote yatokanayo na Nguruwe. Aidha Maje alisema ugonjwa huo unaenezwa na kirus na husababazwa kwa hewa na hivyo kuna hatari ya wafugaji wakapoteza nguruwe wote ndani
ya wilaya maaeneo ugonjwa uliko iingia. Kwa asili ya ugonjwa huu hauna dawa wala kinga na hivyo ukiingia eneo Fulani hakuna njisi, pia kuna wasiwasi wafugaji wanaweza kupoteza nguruwe wote katika maeneo ugonjwa ulipo ingia. Hata hivyo Maje alisema kutokana na ugonjwa huo umeweza kuadhiri uchumi wa mwananchi na halmshauri kwa kodi zilizo kuwa ninalipwa na wafanyabiashara wa mabucha ya nguruwe na ushuru wa majichio.
Pia aliwataka Wafugaji kuweza kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kuwa na sauti ya pamoja na katika kuzikabili changamoto za mifugo ikiwemo kinga kwa wanyama wao na matibabu pindi ugonjwa utokeapo. Pia maje alitumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kuzika mizoga ya nguruwe wanao kufa au kuteketeza kwa moto ili kuogopa ugonjwa huo kuendelea kuenea katika maeneo mengine ndani mkoa wa Dodoma.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.