Wednesday 4th, February 2026
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo Desemba 1,2025 imefanya mkutano wa Baraza la kwanza la Madiwani na kuhudhuriwa na Wananchi mbalimbali.
Wakati wa Mkutano huo wa kwanza wa baraza la Madiwani,madiwani wateule walikuwa viapo chini ya Hakimu Mkaazi Wilaya Ndg Timothy,pia kupata tamko la kiutumishi chini ya Bi Jasminin kutoa Tume ya Maadili na Utumishi wa Umma.
Halikadhalika,umefanyika uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Makamo wake,ambapo Mhe Richard Maponda aliibuka Mshindi wa uchaguzi huo akipata kura zote 44 za ndio na kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri,pamoja na hayo Mhe Baraka habari nae aliibuka mshindi kwa kupata kura zote 44 za ndio na kuchaguliwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa halmashauri.
Hatahivyo,Mwenyekiti wa halmashauri Mhe Maponda pamoja na Makamo wake Mhe Baraka waliwashukuru sana madiwani kwa kuwaamini nankuwapigia kura ili waweze kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya Halmashauri.







Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.