Mradi wa Umaliziaji wa Zahanati ya Kitati una thamani ya Tsh 21,000,000.00. Fedha hizo ni za ruzuku ya miradi ya maendeleo iliyotolewe na serikali. Ujenzi upo katika hatua nzuri ya umaliziaji ambapo fedha hizo zimetumika kununua vifaa vya dari, kuweka milango na madirisha na kupiga plasta. Mpaka sasa dari imewekwa zoezi la kupaka rangi na kuweka madirisha na milango linaendelea.
Mradi wa Ujenzi wa madarasa 3 katika Shule ya msingi Kidenge, mradi wenye thamaniya Tsh 20,000,000.00. Fedha hizo ni za ruzuku ya miradi ya maendeleo iliyotolewe na serikali Ujenzi upo katika hatua ya kumwaga jamvi. Mradi huu unaendelea vizuri
Mradi wa umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha Afya Winza mradi wenye thamani ya Tsh 34,000,000.00 ujenzi upo katika hatua ya umaliziaji wa dari, rangi, milango, madirish, miundombinu ya umeme.
Mradi wa Ujenzi wa Bara bara ya Lumuma Mbuga Wenye thamani ya Tsh 640,000,000. Mpaka sasa Mkandarasi yupo uwandani anaendelea na kazi.
Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 3 katika shule ya Msingi Chinyika. Mradi huu una thamani ya Sh 81,000,000. Mradi huu upo katika hatua za Awali ambapo Mhandisi anaandaa michoro na makadirio ya Gharama za Ujenzi (BOQ)