Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri anawatangazia wananchi wote wa Wilaya ya Mpwapwa Kuwa tarehe 12 Agosti, 2019 Wilaya yetu inatarajia kuupokea MWENGE WA UHURU wenye Ujumbe: "MAJI NI HAKI YA KILA MTU, TUTUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA".
Mwenge huo utatokea Wilaya ya Kongwa na Utapokelewa katika Kijiji cha Nghambi kata ya Nghambi. Kwa mwaka huu 2019 MWENGE WA UHURU unatarajiwa kukimbizwa Wilayani hapa na utakuwa na shughuli ya kuona miradi miwili nayo ni Ujenzi wa Wodi ya Utapia Mlo katika hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na Ufugaji wa Nyuki katika Hifadhi ya Msitu wa Kwa Mshango na Kuzindua miradi mitatu nayo ni: Miundombinu ya Mnada wa Wanyama - Ilolo, Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mzase kata ya Berege, na Maktaba ya Shule ya Sekondari Kibakwe kata ya Kibakwe. Miradi yote mitano ina jumla ya thamani ya Tshs.693,268,640.89.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.